Afghanistani-Ufaransa

Askari wawili wa Ufaransa wauawa nchini Afghanistani

Askari wa ufaransa nchini Afghanistani
Askari wa ufaransa nchini Afghanistani RFI

Wanajeshi wawili raia wa Ufaransa ambao wanashika doria nchini Afghanistan katika Jeshi la Kujihami la Nchi za Magharibi NATO wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa na mtu mwenye silaha ambaye alikuwa amevaa sare za kijeshi ambae aliuawa baada ya kutekeleza mauaji hayo. Idadi hiyo imepelekea idadi ya wanajeshi wa Ufransa waliuawa nchini Afghanistani kufikia 78.

Matangazo ya kibiashara

NATO imethibitisha kutokea kwa vifo hivyo huku wanajeshi wengine wawili wakijeruhiwa kwenye shambulizi hilo lililotokea katika Bonde la Tagab na tayari ofisi ya rais wa Ufaransa imekiri kutokea kwa vifo hivyo.

Tayari Kundi la Wanamgambo wa Taliban limejigamba kutekeleza shambulizi hilo lililotekelezwa katika Jimbo la Kapisa lililopo Mashariki mwa Mji Mkuu Kabul na Ofisi ya Rais Nicolas Sarkozy imesema licha ya vifo hivyo wataendelea kuimarisha amani na usalama.

Katika maandalizi ya kuviondowa vikosi vya kigeni nchini Afhanistani jeshi la nchi hiyo limekuwa likiajiri askari huku na kule ambao wanafunzwa na kikosi hicho cha Ufaransa.

Mwezi Julai iliopita katika kijiji cha Joybar, mtu mmoja alievalie sare ya polisi ya Afghanistani alijilipua na kuwauawa ma komando watano kutoka Ufaransa.