Syria

Watu 13 wauawa nchini Syria wakati tume ya waangaliz wakizuru maeneo kadhaa ya jiji la Homs

Sur cette capture de vidéo postée sur Youtube on voit des observateurs de la Lige arabe en gilet orange à Homs le 27 décembre 2011
Sur cette capture de vidéo postée sur Youtube on voit des observateurs de la Lige arabe en gilet orange à Homs le 27 décembre 2011 AFP/Youtube

Mapigano mapya yaripotiwa nchini Syria ambapo watu zaidi ya 13 wameuawa na vikosi vya serikali kwenye miji mbalimbali nchini humo. Waangalizi kutoka Umoja wa nchi za Kiarabu wamezuru juzi na jana maeneo mbalimbali ya mji wa Homs kwaajili ya kufanya uchunguzi wa tuhuma za kuwepo ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na pande zote mbili. Serikali ya Syria imetangaza hapo jana kuwaacha huru wafungwa 755, ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kurejesha utulivu nchini humo. Hata hivyo Ufaransa imeanza kukemea hatuwa ya wachunguzi hao ya kuridhishwa na hali inayo endelea nchini humo kwa muda mfupi.

Matangazo ya kibiashara

Hatimae waangalizi wa Jumuia ya nchi za Kiarabu wameruhusiwa kutembelea miji inayo shuhudiwa machafuko makubwa jijini Homs ambako wananchi wa maeneo hayo waliwataka wajumbe hao waelekea katika eneo hilo kushuhudia mauaji yaliotekelezwa na vikosi vya serikali.

Wananchi walijitokeza kwa wingi huku wakitowa kauli mbiu za kuipinga serikali ya rais Bashar al Assad na kuonyesha maiti za watoto na watu wazima, pamoja pia na mabaki ya risase zilizo tumiwa na wanajeshi wa serikali.

Kiongozi wa waangalizi hao jenerali Mohammed al-Dabi alitangaza siku moja baada ya kuzuru jiji la Homs kwamba hali ni tulivu, jambo ambalo limepingwa vikali na wapinzani pamoja na mashirika yanayo tetea haki za binadamu waliosema kwamba kauli hiyo haina ukweli wowote kwani, wananchi wengi waliuawa na wanajeshi wazoefu wa kulenga.

Antonio Valero msemaji wa ikulu ya Ufaransa Quai d'Orsay, amesema kuwa, anamatumaini kwamba mkuu wa tume hiyo ya wajumbe wa Jumuia ya nchi za kiarabu atarejelea kauli yake baada ya kukutana na pande mbalimbali na kuzuru maeneo ya baba Amro jijini Homs kuliko ripotiwa mauaji makubwa.