SYRIA

Waandamanaji nchini Syria waupokea mwaka mpya kwa maandamano.

Maelfu ya waandamanaji  nchini Syria
Maelfu ya waandamanaji nchini Syria REUTERS/Handout

Waandamanaji wamasuala ya demokrasia nchini Syria wameupokea mwaka mpya kwa maandamano na kushuhudia mtoto mmoja akiwa wa kwanza kupoteza maisha kwa mwaka huu katika machafuko yanayoendelea nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Waangalizi wa haki za binadamu nchini Syria wamesema kuwa mtoto huyo mwenye umri wa miaka saba ameuwawa katika jimbo la Hama baada ya risasi kupiga katika gari alimokuwa.

Wakati huohuo waangalizi wa jumuiya ya nchi za kiarabu wametembelea maeneo kadhaa ya machafuko nchini humo,ambapo mgogoro umejitokeza baada ya mmoja wa waangalizi hao kutajwa kuishutumu serikali kwa kutuma vibaraka wao na kutaka wao waondolewe.