YEMEN

Serikali ya Yemen yamsamehe rais Ali Abdullah Saleh

Raisi wa Yemen,Ali Abdullah Saleh
Raisi wa Yemen,Ali Abdullah Saleh

Serikali ya mpito ya Yemen imekubali kumsamehe kiongozi wa taifa hilo, Ali Abdullah Saleh, hatua inayofungua milango kwa kiongozi huyo kuondoka madarakani ukiwa mpango wa jumuia ya nchi za Ghuba kumaliza maandamano ya muda mrefu dhidi ya utawala wake.

Matangazo ya kibiashara

Salleh na wasaidizi wake wa karibu waliokuwa pamoja katika serikali,idara za kiraia na kijeshi wamepewa msamaha huo kisheria.

Baraza la umoja wa kitaifa linaloongozwa na upinzani limesema mswada huo wa sheria unatarajiwa kupelekwa bungeni ili kuidhinishwa.

Mnamo mwezi Novemba Saleh alitia saini mapendekezo ya kumaliza mzozo wa kisiasa nchini Yemen, na hivi sasa anashikilia wadhifa wa urais mpaka pale uchaguzi utakapofanyika mwezi ujao.