SYRIA-UTURUKI

Waziri mkuu wa Uturuki Recep Tayyip aonya kutokea vita vya wenyewe kwa wenyewe syria

Waziri mkuu wa Uturuki,Recep Tayyip Erdogan
Waziri mkuu wa Uturuki,Recep Tayyip Erdogan Reuters

Waziri Mkuu wa Uturuki,Recep Tayyip anaonya kuwa huenda kukatokea vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa kutokana na mauji yanayoendelea dhidi ya waandamanaji. 

Matangazo ya kibiashara

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu elfu tano wameuawa katika machafuko hayo yenye miezi kumi sasa tangu kuanza nchini humo.

Wakati huu waangalizi kutoka nchi za kiarabu wameidhinishwa kuwepo nchini humo kutathmini machafuko hayo.

Rais Bashar AL-Asaad ambaye waandamanaji wanamtaka ajizulu,anatarajiwa kuzungumzia machafuko yanayoendlea nchini humo wakati wowote.