AFRIKA KUSINI

Daktari Nkosazana Dlamini-Zuma aendeleza kampeni kutwaa nafasi kuongoza Umoja wa Afrika.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini daktari Nkosazana Dlamini-Zuma
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini daktari Nkosazana Dlamini-Zuma defenceweb.co.za

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Afrika Kusini daktari Nkosazana Dlamini-Zuma ameendelea na kampeni zake za kuhakikisha anatwaa nafasi ya kuwa mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika AU nafasi ambayo kwa sasa inashikiliwa na Jean Ping.

Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi wa nafasi hiyo unatarajiwa kufanyika juma lijalo pale ambapo mkutano wa Umoja wa Afrika utafanyika ambapo Ping anamaliza muda wake na hivyo uchaguzi utafanyika kujaza nafasi yake.

Waziri wa Mambo ya nje wa Afrika Kusini Maite Nkoana-Mashabane amesema wanaamini daktari Dlamini-Zuma atafanyakazi kwa uadilifu mkubwa kama ambayo ilifanywa na mtangulizi wake Ping.