RWANDA

Serikali ya Rwanda yawakamata na kuwasimamisha kazi Majenerali wanne wa Jeshi la nchi hiyo.

Ramani ya nchi ya Rwanda ikipakana na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
Ramani ya nchi ya Rwanda ikipakana na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo world atlas.com

Serikali ya Rwanda imewakamata na kuwasimamisha kazi Majenerali wanne wa Jeshi la nchi hiyo kwa kosa la kufanya biashara na raia kwenye eneo la mpaka wa taifa hilo la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Jeshi Kanali Joseph Nzabamwita amethibitisha kukamatwa kwa majenerali hao wanne na kusema kuwa wamekuwa wakijihusisha na biashara haramu katika eneo hilo.

Kanali Nzabamwita amewataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Luteni Jenerali Fred Ibingira, Jenerali Richard Rutatina, Brigedia Jenerali Wilson Gumisiriza na Kanali Dan Munyuza.

Aidha Kanali Nzabamwita amesema kwa sasa uchunguzi unafanyika kubaini ni kwa nini Majenerali hao walidiriki kufanya biashara kinyume na kazi yao inavyowataka kufanya.