UJERUMANI-SYRIA

Ujerumani yaishutumu Urusi dhidi ya Syria.

Balozi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa UN Peter Wittig
Balozi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa UN Peter Wittig unmultmedia .org

Ujerumani imejitokeza na kuishutumu vikali Urusi kutokana na kuzuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN kuchukua hatua dhidi ya Syria kwa lengo la kumaliza umwagaji damu ambao unaendelea kushuhudiwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Balozi wa Ujerumani katika Umoja wa Mataifa UN Peter Wittig amesema kuwa wanachama kumi na watano wa Baraza la Usalama hawawezi kukaa kimya kwani ni jukumu lao kuhakikisha wanamaliza machafuko hayo.

Balozi Wittig amechukizwa na hatua ya Urusi kufananisha mjadala wa Syria na mashambulizi ya majeshi ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO ambayo yalifanyika nchini Libya.