ZIMBABWE

Wafanyakazi nchini Zimbabwe wapuuza mwito wa mgomo.

thezimbabwean.co.uk

Idadi kubwa ya wafanyakazi wa umma nchini Zimbabwe wamefika kazini kama kawaida licha ya muuungano wa vyama vya wafanyakazi nchini humo kuitisha mgomo wa siku moja kulalamikia nyongeza ya mshahara.

Matangazo ya kibiashara

Jijini Harare shughuli ziliendelea kama kawaida huku wafanyakazi wakienda ofisini na wafanyabiashara kufungua biashara zao.

Muungano huo wa wafanyakazi ulitaka wafanyakazi wote wa serikali kusalia nyumbani leo,katika juhudi zao za kushinikiza serikali kuwaongezea mshahara kutoka dola mia mbili hadi dola mia tano,nyongeza ambayo serikali ya Zimbabwe inasema haiwezi kumudu.

Mgomo wa wafanyakazi wa umma umekuwa ukishuhudiwa nchini humo tangu mwaka 2007.