AFGHANISTANI

Wanajeshi sita wa Marekani wauwawa nchini Afghanistani.

Baadhi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan
Baadhi ya wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan frumforum.com

Wanajeshi sita wa Marekani ambao wanalinda amani nchini Afghanistan wamepoteza maisha kwenye ajali ya helkopta ambayo imetokea Kusini mwa nchi hiyo ikiaminika imefanikishwa na maadui wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la kujihami la nchi za Magharibi NATO ambalo linaongoza operesheni ya kushika doria nchini Afghanistan imethibitisha kutokea kwa vifo hivyo vya wanajeshi sita wa Marekani na imesema uchunguzi umeanza kubaini chanzo chake.

Naye afisa mmoja wa jeshi la Marekani huko Afghanistan amekanusha chanzo cha ajali ya helkopta hiyo ni kudunguliwa ikiwa angani na wabaya wa nchi hiyo lakini anahofia kulikuwa na tatizo la kiufundi.