DR CONGO

Matokeo ya uchaguzi wa wabunge yatangazwa DR Congo

Raisi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Joseph Kabila,pembeni ni kiongozi wa upinzani Etiene Tshekedi
Raisi wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo,Joseph Kabila,pembeni ni kiongozi wa upinzani Etiene Tshekedi

Chama tawala nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo PPRD kimejinyakulia idadi kubwa ya viti huku muungano wa upinzani unaomuunga mkono Etiene Tshekedi ukiachwa mbali katika Matokeo ya uchaguzi wa wabunge.

Matangazo ya kibiashara

Tume huru ya uchaguzi huko Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo imetumia miezi miwili kukusanya matokeo ya kura hizo za ubunge uliofanyika kipindi cha uchaguzi mkuu na kutangaza matokeo hayo ya viti 432 vya ubunge.

Idadi ya wanawake inaonekana kuwa ndogo miongoni mwa wabunge waliochaguliwa, huku baadhi matokeo ya viti sitini na nane hayakutangazwa hasa katika mji mkuu kinshasa.

Tume hiyo ya uchaguzi imesema majina ya washindi yatachapishwa juma lijalo huku kwa mujibu wa taarifa za awali ndugu wawili wa raisi Joseph Kabila ni miongoni mwa wabunge wateule.