SYRIA

Vikosi vya rais Assad vyaendeleza mashambulizi dhidi ya waandamanaji katika mji wa Homs.

REUTERS/Handout

Vikosi vya askari wanaomuunga mkono rais Bashar al Assad bado vimeendeleza mashambulizi makubwa dhidi ya waandamanaji katika mji wa Homs huku maelfu ya raia wakiendelea kuandamana kupinga utawala wake.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waangalizi wa haki za binadamu nchini humo waandamanaji walijitokeza kutoka katika miskiti baada ya swala ya Ijumaa, huku wengine wakitokea Damascus kufuatia wito wa wanaharakati kupitia mtandao ukiwataka kuanza hatua mpya ya maandamano.

Wakiwa katika mkusanyiko mkubwa waandamanaji hao walisikika wakipiga kelele za kumtaka rais Bashar Al Assad kuondoka madarakani.