Afghanistani-Marekani

Marekani yaomba radhi kutokana na kuchomwa kwa Quran nchini Afghanistani

Vurugu za zuka baada ya wanajeshi wa Marekani kuchoma moto Quran
Vurugu za zuka baada ya wanajeshi wa Marekani kuchoma moto Quran REUTERS/Ahmad Masood

Serikali ya Marekani imeomba radhi kutokana na kuchomwa kwa Quran nchini Afghanistan kulikofanywa na wanajeshi wa nchi hiyo wakati huu ambapo maandamano ya wananchi wenye hasira yakiendelea kupinga uwepo wa Majeshi ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta amesema tukio hilo ni la bahati mbaya na kumuagiza Kamanda wa Vikosi vyake nchini Afghanistan Jenerali John Allen kufanya uchunguzi kubaini chanzo cha kuchomwa kwa Quran.

Jenerali Allen tayari ameshaomba radhi kwa kile ambacho kimetokea nchini humo huku Rais Hamid Karzai akitaka uchunguzi ufanyike mara moja kujua sababu zilizochangia kuchomwa kwa Quran.

Naye msemaji wa ikulu ya Marekani Jay Carney amesema serikali ya Marekani imeomba radhi kwa tukio hilo lililojitokeza la kipekee ambalo amesema ni la bahati mbaya na halionyeshi tabia njema ambayo wanayo wanajeshi wa Marekani kwa dini ya watu wa Afghanistani.

Viongozi wa jeshi la ISAF wanaendelea na uchunguzi kujua nini kilichotokea na kuhakikisha hatua zinachukuliwa ili tukio kama hili lisitokee tena.

wananchi wa Afghanistani waliokuwa na hasira wameandamana kupinga kitendo hicho cha askari wa Marekani kuichoma Quran takatifu. Machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu watano