Yemeni

Wanamgambo watano wa Al Qaeda wauawa nchini Yemen

Wafuasi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda
Wafuasi wa kundi la wanamgambo wa Al Qaeda

Wanamgambo watano wa Al Qaeda wameuawa katika shambulio la Anga katika Gari jimboni Bayda nchini Yeman hii leo, tukio lililotokea baada ya kuwepo machafuko katika eneo hilo wakati kikosi cha anga kikishambulia maeneo ya wanamgambo hao karibu na eneo la Abyan.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa kikabila katika eneo hilo amethibitisha kutokea kwa Shambulio hilo, lililotokea baada ya maafisa usalama kusema kuwa askari watatu wameuawa katika Shambulio la Bomu la kujitoa muhanga mapema hii leo.
 

Maafisa wa Kijeshi wamesema kikosi cha anga pia kilifanya mashambulizi katika Ngome za Al Qaeda ikiwemo kambi iliyoshukiwa kuwa ya Mafunzo karibu na jimbo la Abyan, ambapo kulitokea shambulio katika kambi ya jeshi na kusababisha wanajeshi 185 kupoteza maisha.

Mashambulio ya hii leo ni miongoni mwa mashambulizi yanayofanywa na mtandao wa Al Qaeda dhidi ya vikosi vya Yemen ambavyo vimekuwa vikipambana nao tangu baada ya kuondoka madarakani kwa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Ali Abdullah Salleh.