Syria

Mapigano yazuka nchini Syria, Marekani yaelekeza nguvu UN

Reuters/路透社

Mashambulizi mapya yameibuka nchini Syria wakati huu ambapo serikali ikiwa imeahidi kutekeleza mapendekezo sita ya Mjumbe wa Umoja wa Mataifa UN na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Kofi Annan lengo likiwa ni kudhibiti umwagaji wa damu katika nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yanatajwa kuchangia vifo vya watu thelathini na wanane wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa UN unajiandaa kutuma waangalizi wao kujionea hali ilivyo na kuanza kupeleka misaada.

Marekani kupitia kwa Balozi wao katika Umoja wa Mataifa UN Susan Rice imesema inaimani na Baraza la Usalama ndilo linaweza kumaliza kile ambacho kinaendelea huko Damascus kama anvyoeleza.

Kama hiyo haitoshi Marekani imeongeza shinikizo zao kwa serikali ya Syria na hapa Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Victoria Nuland anasema wote waliotenda makosa watakumbana na mkono wa sheria.

Serikali ya Syria ilisema itakuwa imetekeleza mapendekezo sita ya Kofi Annan kufika tarehe kumi ya mwezi huu ikiwemo ni pamoja na kusitisha mapigano na kuondoa vifaru uraiani.