KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini inajiandaa kufanya majaribio yake makombora yake ya masafa marefu wakati Korea Kusini ikijipanga Kijeshi

Makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini ambayo yanatarajiwa kujaribiwa baadaye mwezi huu
Makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini ambayo yanatarajiwa kujaribiwa baadaye mwezi huu

Korea Kaskazini inajiandaa kufanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu tarehe kumi na mbili au kumi na sita ya mwezi huu wakati huu ambapo Korea Kusini ikiendelea kutoa onyo kwa jirani zao kutothubutu kutekeleza mpakngo wake huo kwa sasa.

Matangazo ya kibiashara

Korea Kaskazini imejiapiza kufanya majaribio hayo kwani mipango yao imeshakamilika kwa kila hatua na sasa wapo katika nafasi nzuri ya kuonesha nguvu walizonazo hasa kwenye umiliki wa silaha za makombora ya masafa marefu baada ya kufanya hivyo kwa makombora ya masafa mafupi.

Waandishi ambao wameshiriki kwenye utengenezaji wa makombora hayo ya masafa marefu wamesema kazi yao imefanikiwa kwa kiwango kikubwa sana kwani walifanya uchunguzi wa kina kabla ya kutengeneza makombora hayo ambayo yamekuwa gumzo kwa sasa.

Marekani na nchi nyingine jirani na Korea Kaskazini ambazo zipo kwenye eneo la Peninsula zimeendelea kutilia shaka mno majaribio hayo ya makombora ya masafa marefu kwani yanakwenda kinyume na Azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Pyongyang imekuwa ikizuiliwa kwa kiwango kikubwa kutekeleza majaribio ya aina yoyote ya silaha zake za masafa marefu kwa kuwa inaonekana inaweza kuwa kitisho kwa dunia kwani mataifa mengine yanaweza kutekeleza suala kama hilo.

Korea Kusini kupitia Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Kim Min-seok amesema wanajipanga vyema katika kukabiliana na kitisho hicho kipya cha kutekeleza majaribio ya makombora yake ya masafa marefu.

Serikali ya Seoul imesema wamejiandaa vyema kijeshi kukabiliana na Korea Kaskazini kipindi hiki ambacho eneo la Peninsula limeanza kukumbwa na hofu kubwa iwapo majaribio hayo ya masafa marefu yatatekelezewa.

Korea Kusini na China zimeonesha wasiwasi wa mipaka yao kama itakuwa salama kutokana na jaribio hilo na hivyo kutishia kuiangushia silaha hizo ikiwa zitavuka mipaka na kuingia kwenye eneo lao.

Jaribio la makombora ya masafa marefu ya Korea Kaskazini yanakuja wakati huu ambapo maadhimisho ya miaka mia moja ya Kiongozi wa zamani wa Taifa hilo Comrade Kim Il-Sung yakifanyika.