OSLO-NORWAY

Anders Breivik amaliza utetezi wake akidai mauaji aliyofanya yalilenga kuilinda nchi yake

Wanasheria wa Breivik wakiteta jambo wakati kesi hiyo ikiwa imesimama kwa muda hii leo
Wanasheria wa Breivik wakiteta jambo wakati kesi hiyo ikiwa imesimama kwa muda hii leo REUTERS/Fabrizio Bensch

Mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 nchini Norway, Anders Breivik amemaliza kutoa utetezi wake huku akisisiza kuwa mauaji aliyoyafanya yalikuwa yanaweza kuepukika. 

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kwa kujiamini, Breivik amesema kuwa matukio aliyoyatekeleza yalilenga kuilinda nchi yake na wananchi wake ambao wamevamiwa na watu ambao hawaitakii mema nchi yake na Umoja wa Ulaya.

Breivik ameenda mbali zaidi na kusema kuwa mauaji aliyoyafanya laiyapanga kwa muda mrefu na kwamba hajawahi kufanyika toka kumalizika kwa vita vya kwanza vya dunia kwaajili ya utetezi wa rais wenzake.

Hata hivyo wakati kesi hiyo ikiendelea, jaji mkuu anayesikiliza kesi hiyo alilazimika kumtoa nje jaji mmoja baada ya kubainika kuwa mara baada ya Breivik kutekeleza mauaji yale aliandika kwenye mtandao wa kijamii kuwa mtuhumiwa huyo ahukumiwe kifo.

Kauli yake ilizua utata bungeni ambapo upande wa utetezi ilitaka jaji huyo aondolewe kwakuwa tayari alikwishamuhukumu mteja wake kwa kutaka mahakama itoe adhabu ya kifo kwa mtuhumiwa.

Jaji Thomas Indreboe ambaye alikuwa mmoja kati ya majaji watano waliochaguliwa kusikiliza kesi hiyo aliandika kuwa suluhisho pekee la kumaliza simanzi ya ndugu waliopoteza ndugu zao kwenye mauaji hayo ni adhabu ya kifo jambo ambalo limeelezwa kuwa angeendelea kuwepo asingekuwa wazi kutoa hukumu juu ya kesi hiyo.