OSLO-NORWAY

Upande wa mashtaka wamuhoji Breivik huku mara kadhaa akikataa kujibu maswali

Mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 nchini Norway, Anders Breivik akiwa mahakamani
Mtuhumiwa wa mauaji ya watu 77 nchini Norway, Anders Breivik akiwa mahakamani Reuters

Mtuhumiwa mkuu wa mauaji ya watu 77 nchini Norway kwenye mji wa Oslo na visiwa vya Utoeya, Anders Breivik ameanza kuhojiwa na upande wa mashtaka kuhusiana na matukio aliyoyatekeleza. 

Matangazo ya kibiashara

Hii leo mara baada ya kufikishwa mahakaman, Breivik alikuwa tofauti na jana ambapo hii leo mara kadhaa mtuhumiwa huyo alikataa waziwazi kujibu maswali ya mwendesha mashtaka.

Moja ya mwaswali aliyoulizwa hii leo na mwendesha mashtaka wa serikali ni uhusiano alionao na kundi la mrengo wa kulia la Knights Templar, kundi ambalo mara zote Breivik amekuwa akihusishwa nalo.

Lakini wakati akiulizwa swali hilo aligeuka mkali na kukataa kujibu endapo anauhusiano nalo au la.

Majaji wa mahakama hiyo hii leo pia wamelezwa na mwendesha mashtaka kuwa kundi ambalo amelitaja Breivik kuwa na uhusiano nalo halijulikani na halipo kwahivyo anatumia mwavuli wa kudni hilo kuficha mabaya aliyoyafanya.

Kabla ya kutekeleza shambulio hilo Breivik alituma kwenye mtandao nyaraka zaidi ya 1500 alizodai ni za kundi ambalo analitumikia linalopinga Uslamu nchini Norway.

Taarifa kutoka ndani ya mahakama hiyo zinasema kuwa lengo la maswali hayo kwa mtuhumiwa huyo, ni kutaka kuionyesha mahakama kuwa Breivik sio mtu wa kuaminika hata kwenye ushahidi wake.

Tofauti na wakati kesi hiyo ikianza hii leo pia walikuwepo vijana ambao walinusurika kwenye shambulio la kwenye kisiwa cha Utoeya.