SUDAN

Raia wa kigeni wakamatwa ndani ya mpaka wa Sudani

Msemaji wa jeshi la Sudan, Sawarmi Khaled Saad, akizungumza na waandishi wa habari
Msemaji wa jeshi la Sudan, Sawarmi Khaled Saad, akizungumza na waandishi wa habari Reuters

Raia wanne wa kigeni wanaofanya uchunguzi juu ya machafuko yanayoendelea baina ya Sudan na Sudan Kusini wamekamatwa katika eneo la mafuta huko Heglig,serikali ya Khartoum imearifu.

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa jeshi la Sudan Sawami Khaleed Saad amethibitisha kuwa raia hao wanne wamepelekwa mjini Khartoum kwa uchunguzi zaidi na kuongeza kuwa Sudan Kusini imekuwa ikifanya uhalifu dhidi yao kwa usaidizi wa wataalamu kutoka nchi za nje.

Taarifa ya jeshi ilibainisha majina ya waliokamatwa ndani ya mipaka ya Sudan ni Briton raia wa Norway na wengine ni raia wa Afrika ya Kusini na Sudan Kusini.

Wakati ugomvi baina ya nchi hizo ukiendelea serikali ya China imekubali kuiwezesha Sudan kusini kwa mkopo wa dola za Marekani bilioni 8 kwa ajili ya maendeleo ya miundo mbinu nchini humo.