MYANMAR

Katibu Mkuu wa UN Ban apongeza kitendo cha Kiongozi wa Upinzani nchini Myanmar Suu Kyi kula kiapo kuwa Mbunge

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon amempongeza Kiongozi wa Upinzani na Mwanademokrasia nchini Myanmar Aung San Suu Kyi kutokana na kitendo chake cha kuamua kula kiapo cha kuwa Mbunge baada ya hapo awali yeye na wabunge wengine wa chama chake kukataa kuapishwa.

Kiongozi wa Upinzani Nchini Myanmar Aung San Suu Kyi akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika huko Yangon
Kiongozi wa Upinzani Nchini Myanmar Aung San Suu Kyi akiwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban Ki Moon kwenye mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika huko Yangon
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu Ban ametoa kauli hiyo alipokutana na Mshindi huyo wa Tuzo ya Amani ya Nobel Suu Kyi na kusema yeye kweli ni Kiongozi kutokana na kuweka maslahi ya Taifa mbele na hivyo kuamua kubadili msimamo wake wa awali.

Ban ameweka bayana kuwa uamuzi ambao aliuchukua Suu Kyi siku ya jumatatu ulikuwa mgomu sana lakini ameonesha namna ambavyo yupo tayari kuwatumikia wananchi katika kuhakikisha demokrasia ya kweli inapatikana nchini mwake.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN ameongeza kuwa Kiongozi ambaye yupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi lazima awe na uwezo wa kubadili mawazo yake kwa maslahi ya wale ambao wamemchagua.

Suu Kyi naye akimjibu Katibu Mkuu Ban amemwambia wao katika Chama Chao Cha NLD wanaamini katika mabadiliko hivyo kitu muhimu kwao ni kuweka maslahi ya taifa kwanza kabla ya kufanya kitu chochote.

Suu Kyi amesema kutokana na hilo ndiyo maana yeye na wabunge wengine wa Chana Cha NLD wakabadili uamuzi wao siku ya jumatatu na hivyo kula kiapo cha kuwa wabunge ili waweze kupambana katika kufanya mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo.

Ban pia ameitaka serikali ya Myanmar kuhaklikisha inafanya mababiliko ya haraka ili waweze kuendana na mabadiliko ya kidemokrasia yanayotakiwa na Jumuiya ya Kimataifa baada ya kuondolwe kwa Utawala wa Kijeshi.

Mapema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN Ban ameyaomba Mataifa ya Magharibi kuondoa vikwazo kwa nchi hiyo ili iweze kufanikiwa kwenye harakati zake za kufanya mabadiliko ya kidemokrasia ambayo yanashinikizwa na Upinzani.