Mamia wajeruhiwa katika maandamano mjini Cairo,Misri
Imechapishwa:
Mtu mmoja amethitika kupoteza maisha na mamia wakijeruhiwa katika mji mkuu wa misri,Cairo baada ya majeshi yenye silaha kutumia nguvu kuwasambaratisha waandamanji waliokuwa wakikaribia wizara ya ulinzi nchini humo.
Ahmed Ansari ni kiongozi wa huduma ya kwanza amesema watu wengi wamejeruhiwa vibaya na kusambazwa katika hospitali mbalimbali mjini Cairo.
Mapigano hayo makali kati ya polisi na raia wanaoandamana yalisababisha baraza la serikali ya kijeshi nchini humo kutoa amri ya kutotoka nje wala kukaribia eneo la maandamano.
Maandamano hayo yanakuja huku kukitajwa kuwepo kwa hofu ya uchaguzi kutawaliwa na upendeleo kwa mgombea wa serikali ya kijeshi huku wengine wakisema hawana imani na baraza kuu la serikali ya kijeshi kama litaridhia kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.