DRC

Jeshi nchini DRC ladai kumaliza operesheni zake kaskazini mwa nchi hiyo

Kiongozi wa jeshi la DRC anayetafutwa Jenerali Bosco Ntaganda
Kiongozi wa jeshi la DRC anayetafutwa Jenerali Bosco Ntaganda Reuters

Jeshi la Jamuhuri ya Congo limesema kuwa limemaliza Opereshaeni yake mashariki mwa nchi hiyo, ambapo limeeleza kuwa limefanikiwa kudhibiti eneo hilo. 

Matangazo ya kibiashara

Vikosi vya Congo vimekuwa vikipambana na waasi na kumsaka kiongozi wa zamani wa waasi ,Jean Bosco Ntaganda

kwa takriban siku tatu, wakazi wa Bunagana, mji ulio karibu na Rwanda na Uganda ambalo limekuwa likikumbwa na mashanbulizi ya mara kwa mara wamekuwa wakikimbia makazi yao nyakati za usiku na kurejea kukiwa kumekucha.

Mwanzoni mwa juma lililopita wanajeshi wafuasi wa Ntaganda walipambana na vikosi vya Congo mashariki mwa nchi hiyo.

Ntaganda anayetafutwa na mahakama ya kimataifa ya ICC akikabiliwa na makosa ya uhalifu wa kivita ikiwemo kuwatumia watoto katika jeshi na Raia amekuwa akituhumiwa na serikali kwa kuendesha vita kweny mkoa wa kivu ya kaskazini.