SYRIA

Maelfu ya wananchi nchini Syria washiriki uchaguzi mkuu wa wabunge

Baadhi ya mabango ya wagombea ubunge wanaoshiriki uchaguzi nchini Syria
Baadhi ya mabango ya wagombea ubunge wanaoshiriki uchaguzi nchini Syria Reuters

Maelfu ya wananchi wa Syria hii leo wameshiriki zoezi la upigaji kura za viti vya ubunge wa vyama vingi nchini humo, uchaguzi ambao umekosolewa kwa kiasi kikubwa na upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Kura ambazo awali zilipangwa kufanyika Mwezi Septemba mwaka jana ziliahirishwa mpaka May 7 baada ya rais Basahar al-Asad kuahidi kuanzisha mchakato wa mabadiliko.

Uchaguzi huu unakuja wakati ambapo kumekuwa na hali ya machafuko nchi nzima yaliyoanza katikati ya mwezi march mwaka 2011 ambapo takriban watu 11, 100 wengi wao Raia wamepoteza maisha.

Uchaguzi wa hii leo utakuwa wa kwanza kufanyika tangu Syria ilipofanya uchaguzi wa vyama vingi baada ya kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi kwa nguvu ya kura ya maoni kwa ajili ya uundwaji wa katiba mpya na kupelekea kukoma kwa utawala wa miongo mitano ya utawala wa chama cha BAATH.

Vyama tisa viliundwa na saba kati yake hii leo vinawania nafasi za Ubunge, hata hivyo kura hizo haziungwi mkono na baadhi ya wapinzani wakidai kuwa uchaguzi huo unafanyika wakati ambao hali ya usalama ni tete, hali ya mauaji ya kila siku ikiendelea ,mateso na wengine kukimbia makazi yao.

Jumla ya wagombea 7195 wamejiandikisha kuwania viti 250 vya ubunge nchini Syria.