YEMEN-MAREKANI

Makachero wa CIA wafanikiwa kumuua Fahd al Quso mmoja kati ya viongozi wa juu wa kundi la Al-Qaeda

Fahd al Quso kiongozi wa juu wa kundi la Al-Qaeda aliyeuawa nchini Yemen
Fahd al Quso kiongozi wa juu wa kundi la Al-Qaeda aliyeuawa nchini Yemen Reuters

Kiongozi wa juu wa kundi la Al Qaeda aliyekuwa akitafutwa na shirika la upelelezi la Marekani, FBI kwa kuhusika na shambulio la Bomu la mwaka 2000 dhidi ya Meli ya Kivita ya Marekani ameuawa kwa shambulio la anga nchini Yemen. 

Matangazo ya kibiashara

Kikosi maalumu cha CIA cha Marekani kimethibitisha kutekeleza shambulio hilo na kudai kuwa kiongozi huyo aliuawa kwa kombora wakati akijiandaa kuingia kwenye gari yake.

Fahd al Quso alishambuliwa kwa kombora alipotoka nje ya Gari lake na kuuawa sambamba na mfuasi mwingine wa kundi la Al Qaeda, tukio lilitokea katika jimbo la Shabwa.

Kikosi cha upelelezi cha CIA na jeshi la Marekani viilikuwa katika Operesheni ya upelelezi , Operesheni iliyopata baraka kutoka kwa Mamlaka ya Yemen.

Al Quso mwenye umri wa miaka 37 alikuwa kwenye Orodha ya magaidi waliokuwa wakitafutwa , na kutolewa ahadi ya kitita cha fedha cha Dola za marekani milioni tano kwa mtoa taarifa za kusababisha kukamatwa kwake.

Mabaharia 17 waliuawa na 39 kujeruhiwa katika shambulio la mwaka 2000 dhidi ya meli hiyo.