URUSI

Vladmir Putin aapishwa rasmi kama rais wa Urusi

Rais wa Urusi Vladmir Putin hatimaye hii leo ameapishwa rasmi kuchukua ofisi ya rais nchini humo ikiwa ni muhula wake watatu kuteuliwa kushika wadhifa huo akichukua madaraka toka kwa Dimirty Medvedev.

Rais wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Urusi Vladmir Putin Reuters
Matangazo ya kibiashara

Sherehe za kuapishwa kwa Putin zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa nchi hiyo wakiwemo wananchi, sherehe ambazo zilifanyika kwenye ukumbi wa St Andrew mjini Moscow.

Awali kabla ya kuapishwa kwa kiongozi huyo, polisi walikabiliana na waandamanaji jirani na ukumbi wa bunge la nchi hiyo ambapo sherehe hizo zilikuwa zinafanyika wakipinga ushindi wa Putin.

Polisi nchini humo imesthibitisha kuwakamata watu kadhaa kuhusiana na vurugu hizo, na kuongeza kuwa watafunguliwa mashtaka kwa mujibu wa sheria kwa makosa ya kutaka kuharibu utulivu wakati wa sherehe za kuapishwa kwa kiongozi wa nchi.

Wanasiasa wa upinzani nchini humo wamekuwa wakikosoa serikali ya nchi hiyo kwa madai kuwa imekuwa ikiendehswa kimabavu na kama kifalme kutokana na kurithishana madaraka kwa viongozi wa chama cha United Russia.

Rais Putin aliachia madaraka ya urais mwaka 2008 kwa Medvedev na baadae kuteuliwa kuwa waziri mkuu kabla ya mwaka huu kushinda kiti cha urais kwa muhula wa tatu.