UGIRIKI

Vyama viwili vilivyokuwa vinaunda Serikali ya muungano nchini Ugiriki vyapoteza viti vingi vya Ubunge

Evangelos Venizelos kiongozi wa chama cha Pasok ambacho kimepoteza viti vingi vya ubunge nchini Ugiriki
Evangelos Venizelos kiongozi wa chama cha Pasok ambacho kimepoteza viti vingi vya ubunge nchini Ugiriki REUTERS/Yves Herman

Vyama viwili vikubwa nchini Ugiriki ambavyo awali viliunga mkono hatua ya Serikali ya nchi hiyo kuamua kupitisha mpango wa kubana matumizi kukabiliana na mdororo wa kiuchumi nchini humo vimepoteza viti vingi vya ubunge kwenye uchaguzi uliofanyika siku ya Jumapili. 

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa kura ambazo zimekwishahesabiwa mpaka sasa ambapo ni karibu zote, matokeo yanaonyesha kuwa chama cha mrengo wa kati cha New Democracy kimepata asilimia 18.9 ya kura ukilinganisha na mwaka 2009 ambapo kilipata asilimia 33.5.

Chama cha mrengo wa kushoto ambacho kinaunda Serikali ya umoja wa kitaifa cha Syriza kimeuwa cha pili kwa kupata asilimia 16.7 wakati chama cha Pasok kikipata asilimia 13.2 ya kura zoet ambazo zimehesabiwa mpaka sasa.

Chama cha Pasok na New Democracy vimekuwa kwenye Serikali ya muungano toka mwezi wa kumi na moja mwaka jana ambapo kushindwa kwao kunaelezwa kumetokana na sera yao ya ubanaji matumizi.

Kiongozi wa chama cha New Democracy Antonis Samaras amesema kuwa atahakikisha anaunda Serikali ya umoja wa kitaifa ambayo itasaida kuinua uchumi wa taifa hilo pamoja na kuheshimu mkataba wa jumuiya hiyo.

Kiongoziu wa chama cha Pasok ambaye pia aliwahi kuwa waziri wa fedha wa nchi hiyo Evangelos Venizelos ametaka kuundwa kwa serikali ya Umoja ambayo itaweka mbele maslahi ya wananchi kuwanusuru na hali mbaya ya Uchumi.