URUSI-MOSCOW

Rais Putin amteua Medvedev kuwa waziri mkuu wake

Rais Mpya wa Urusi Vladmir Putin akipongezwa na waziri mkuu wake Dimitry Medvedev
Rais Mpya wa Urusi Vladmir Putin akipongezwa na waziri mkuu wake Dimitry Medvedev Reuters

Rais wa Urusi Vladmir Putin amemteua Dimitry Medvedev aliyekuwa rais wa nchi hiyo kuwa waziri mkuu mpya katika Serikali yake.

Matangazo ya kibiashara

Tayari bunge la Duma limekwisha idhinisha jina la waziri mkuu huyo ambaye awali alikuwa akihudumu kama rais wa Urusi ambapo nayeye alichukua madaraka ya urais toka kwa Putin aliyekuwa rais mwaka 2008.

Kuteuliwa kwa Medvedv kuwa waziri mkuu kumeendelea kudhihirisha utawala wa chama kimoja kwenye Serikali ya nchi hiyo kwa viongozi kuendelea na tabia ya kuachiana madaraka pindi mmoja wao anapokuwa kiongozi wa juu.

Viongozi hao kwa pamoja hii leo walihudhuria sherehe maalumu za kuadhmisha kumbukumbu ya kumalizika kwa vita vya pili vya dunia ambapo walikutana kwenye gwaride maalumu lililoandaliwa na wanajeshi mjini Moscow.

Wachambuzi wa masuala ya siasa wanadai kuwa hatua ya viongozi wa chama cha United Russia kuendelea kuachiana madaraka itaendelea mpaka pale nchi hiyo itakapofanyia mabadiliko katiba ya nchi hiyo.