UGIRIKI

Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias kuitisha mazungumzo ya mwisho kuepuka uchaguzi mpya.

ctpost.com

Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias  amepanga kuitisha mazungumzo ya mwisho leo Jumamosi katika jitihada za kuunda serikali ya muungano ya dharura na kuepuka uchaguzi mpya, baada ya vyama vikuu kushindwa kuunda muungano.

Matangazo ya kibiashara

Nchi ya Ugiriki ambayo ina mzigo mkubwa wa madeni inahamanika vikali kutokana na hatua za kubana matumizi zilizowekwa kama masharti ya mkopo wake kwa taasisi ya fedha duniani IMF na Umoja wa Ulaya EU ambapo kwa sasa mgogoro huo unatishia kushindwa kutekelezwa kwa makubaliano na kupelekea nchi hiyo kujiondoa uanachama wa umoja wa Ulaya.

Katika uchaguzi wa wabunge Jumapili iliyopita, nchi hiyo imeshuhudia wapiga kura wakiviadhibu vyama tawala na kuacha mpasuko wa kisiasa ambao umeamsha hamasa ya kufanyika kwa uchaguzi mpya ndani ya wiki kadhaa, huku kukiwa na shinikizo kali la Umoja wa ulaya kuhusu uchumi wa Ugiriki.