SUDANI

Sudani Kusini yaondoa askari wake katika eneo la mpaka la Abyei

en.trend.az

Sudan Kusini imeondoa mamia ya polisi katika eneo la Abyei ambalo linagombewa na Sudan, kabla Baraza la Usalama la umoja wa mataifa halijatoa maamuzi ya mwisho, Msemaji wa Umoja wa Mataifa amesema.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo msemaji huyo Martin Nesirky amesema kuwa Umoja wa Mataifa bado haujathibitisha madai ya Sudani Kusini kwamba ameondoa vikosi vyake katika eneo hilo la mpaka linalogombewa na mahasimu hao wawili.

Abyei ni moja ya maeneo mengi yanayosababisha migogoro mingi kati ya Sudan Kusini na Sudan na kuzipeleka nchi hizo mbili katika vita miezi michache baada ya Sudani Kusini kujitenga.