CHINA

Mvua yaleta maafa China,40 wafariki

Mvua zasababisha mafuriko nchini China
Mvua zasababisha mafuriko nchini China

Takribani Watu arobaini wamepoteza maisha nchini China baada ya mvua kubwa kunyesha kwa kiwango kikubwa maeneo ya milima ya kaskazini magharibi mwa china.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa za serikali kupitia mtandao wake takribani watu 18 hawajulikani walipo katika maeneo tofauti hususan jimbo la Gansu huku tayari 87 ni majeruhi wamewahishwa hospitali kupatiwa matibabu.

Uongozi nchini humo umethibitisha karibia watu elfu 29 na mia tatu wameondolewa katika makazi yao baada ya mvua kunyesha kwa dakika 60 mfululizo na kuhatarisha usalama siku ya alhamisi.

Athari mbalimbali zimetajwa ikiwemo vifo,uharibifu wa miundo mbinu za usafiri,umeme,makazi ya watu mashamba na njia za huduma ya mawasiliano kuharibiwa vibayana mvua hizo.