DRC

waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wadai kuua Wanajeshi 26 wa Serikali ya Nchi hiyo

Kiongozi wa jeshi la DRC anayetafutwa Jenerali Bosco Ntaganda
Kiongozi wa jeshi la DRC anayetafutwa Jenerali Bosco Ntaganda Reuters

Waasi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamethibitisha kuwa imewaua wanajeshi 26 wa nchi hiyo katika mapigano makali karibu na Mpaka wa nchi hiyo na Rwanda.

Matangazo ya kibiashara

Luteni kanali Vianney Kazarana ambaye ni Msemaji wa majeshi ya waasi amesema kulikuwa na mapigano yaliyodumu kwa takriban dakika 30 katika wilaya ya Mbuzi mapigano yaliyotokea siku ya Jumapili.

Kazarana amevishutumu Vikosi vya Serikali kwa kufanya mashambulizi kwa kutumia Vifaru na silaha dhidi ya Raia ambao wengi wao wameyakimbia makazi yao tangu tangu mapambano yalipoanza kupamba moto juma lililopita.

Katika hatua nyingine,wakazi wa Eneo la Mashariki mwa Congo wamekimbia mapigano hayo ambapo zaidi ya watu 10,000 wametorokea nchini Rwanda na Uganda.
 

Mapigano yametokea katika maeneo ya Msitu wa hifadhi ya Virunga, ambapo vikosi vya Jeshi la Congo linaamini kuwa kiongozi wa waasi Bosco Ntaganda na vikosi vyake vimejificha katika eneo hilo.