Burundi

Watu sita wa Familia Moja wauawa na Watu wenye hasira nchini Burundi kwa tuhuma za ushirikina

Ramani inayoonesha eneo la  jimbo la Kirundo Kaskazini mwa Burundi
Ramani inayoonesha eneo la jimbo la Kirundo Kaskazini mwa Burundi

Watu sita wa familia moja wakiwemo watoto wawili wameuawa kaskazini mwa nchi ya Burundi kufuatia kuvamiwa na wananchi wenye hasira kwa tuhuma za kushiriki vitendo vya ushirikina, polisi wamethibitisha.

Matangazo ya kibiashara

Tukio hilo la kushtua limetokea kwenye jimbo la Bwambarangwe ambapo kwa mujibu wa polisi tukio hilo lilitokea baada ya wananchi kumtuhumu mwanamke mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Marthe Kabatesi kujihusisha na ushirikina yeye pamoja na familia yake.

Gavana wa jimbo la Kirundo Reverien Nzigamasabo, amedai kuwa wananchi hao baada ya kufika kwenye nyumba anakoishi Marthe, walimkamata na kuanza kumkata na mapanga na kisha kuwachukua watoto wake wawili wakike pamoja na wajukuu wake na kisha kuwakata shingo.

Suala la imani za kishirikina limeendelea kuwa tatizo katika nchi nyingi barani Afrika ambapo matukiuo kama haya yamekuwa yakiripotiwa sehemu mbalimbali ikiwemo Tanzania, Kenya na Uganda pamoja na nchi za Afrika Magharibi.