UGIRIKI

Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias aendelea na mazungumzo na viongozi wa vyama siasa kujaribu kuunda Serikali ya muungano

Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa nchini humo, kulia ni kiongozi wa chama cha Syriza kilichojitoa kwenye mazungumzo hayo Alexis Tsipras
Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias akizungumza na viongozi wa vyama vya siasa nchini humo, kulia ni kiongozi wa chama cha Syriza kilichojitoa kwenye mazungumzo hayo Alexis Tsipras REUTERS/John Kolesidis

Rais wa Ugiriki Karolos Papoulias anaendelea na mazungumzo na viongozi wa vyama vya siasa nchini humo kuangalia uwezekano wa kuundwa kwa Serikali ya muungano inayoonekana kushindikana kupatikana.

Matangazo ya kibiashara

Toka kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchini humo Jumapili iliyopita hakuna chama ambacho kilifanikiwa kufikisha nusu ya kura kukiwezesha kuunda Serikali, badala yake vyama vya Pasok na kile cha News Domcracy ambavyo vilikuwa kwenye Serikali ya muungano vikijaribu kuunda Serikali bila mafanikio.

Rais Papoulias ametisha mazungumzo hayo ikiwa ni siku ya pili toka ameanzisha mazungumzo hayo na vyama viwili pekee huku chama cha Syriza kikikataa kushiriki kwenye mazungumzo hayo.

Chama cha Syriza kilijitoa kwenye mazungumzo hayo kwa madai kuwa hakiungi mkono hatua ya Serikali ya ubanaji wa matumizi na hivyo kilikuwa kikijaribu kutafuta uungwaji mkono toka kwa vyama vingine kabla ya kushindikana.

Endapo viongozi hao wakashindwa kufikia muafaka wa uundwaji wa Serikali ya muungano basi ni wazi kuwa rais Papoulias atalazimika kuitisha uchaguzi mkuu mwingine.

Wakati mvutano huo wakisiasa ukiendelea, mawaziri wa fedha toka nchi 17 za Umoja wa Ulaya EU wanaokutana mjini Brussels wametaka wanasiasa nchini Ugiriki kuafikiana kuunda Serikali ili kuwezesha nchi hiyo kupatiwa awamu nyingine ya mkopo kunusuru uchumi wake.

Mkuu wa makundi ya nchi za EU Jean-Claude Juncker amesema kuwa licha ya mgogoro unaoendelea nchini Ugiriki ana imani kuwa nchi hiyo haitafikia hatua ya kujitoa na kwamba nchi wanachama ziko tayari kuinusuru nchi hiyo kiuchumi.