Amnesty International yaishutumu Tuareg, majeshi ya Mali na Makundi ya Waislam kukiuka haki za Binaadam
Imechapishwa:
Shirika la kimataifa linalotetea haki za Binaadam, Amnesty International limesema makundi ya waislam wenye msimamo mkali na waasi wa Tuareg waliodhibiti eneo la Kaskazini mwa Mali baada ya Mapinduzi ya Kijeshi wameshiriki vitendo vya ukiukwaji wa haki za Binaadam kama Ubakaji, mauaji na kuwatumia Watoto kwenye jeshi lao.
Ripoti iliyotolewa na shirika hilo imesema Wanajeshi wa Mali pia wameshiriki mauaji, na kufanya hali kuwa mbaya zaidi nchini humo katika kipindi cha miaka 50.
Baada ya miongo miwili ya kumbukumbu ya nchi hiyo kuwa na historia nzuri ya uimara wa Nchi hiyo na Amani, hivi sasa imekumbwa na machafuko ambayo yanaelezwa kuwa mabaya zaidi tangu mwaka 1960.
Watafiti wa shirika la Amnesty International limekusanya Ushahidi kutoka kwa Wanawake na Wasichana ambao wamesema kuwa walibakwa wakati mwingine na kundi kundi la watu wenye silaha kwa wakati mmoja wakiwemo wafuasi wa kundi la MNLA.
Halikadhalika imedhihirishwa uwepo wa Watoto katika Jeshi la Tuareg na wapiganaji wa Kiislam katika Ngazi mbalimbali za makundi hayo.
Shirika limeitaka Mamlaka ya Mali na Makundi ya watu wenye silaha kuruhusu Umoja wa Mataifa na Mashirika mengine ya Misaada ya kibinaadam kuwafikia wakimbizi na watu waliokimbia Makazi hasa katika eneo la Kaskazini.