Marekani

Mwanaharakati wa Nchini China Chen Guangcheng aishutumu Serikali ya China kutishia Maisha ya Familia yake

Mwanaharakati wa China Chen Guangchen
Mwanaharakati wa China Chen Guangchen REUTERS/US Embassy Beijing Press Office/Handout

Mwanaharakati Chen Guangcheng raia wa China ambaye hivi karibuni alikimbia toka nyumbani kwake na kwenda kuomba hifadhi kwenye ubalozi wa Marekani, ameibuka tena na kuituhumu serikali ya Beijing kutishia maisha yake na familia.

Matangazo ya kibiashara

Guangcheng safari hii amepeleka tena shauri lake kwenye ofisi za Ubalozi wa Marekani akitaka kupatiwa msaada na rais Barack Obama ili apataiwe kibali cha kuhamisha familia yake kwenda nchini Marekani.
 

Akizungumza kwa njia ya simu akiwa hospitalini alikolazwa, Chen Guangcheng ameituhumu serikali yake kwa kuendelea kuidhalilisha familia yake kwa kile alichoeleza ni kama kisasi cha Serikali baada ya yeye kuomba hifadhi kwenye ubalozi huo.
 

Mwanaharakati huyo aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 2010 alipokuwa amefungwa baada ya kukosoa sera ya Serikali ya kulazimiasha utoaji mimba na kufunga kizazi.