DR CONGO

Majeshi ya Congo DR yashambulia kambi ya waasi Kivu

saidmihala.blogspot.com

Jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo limeshambulia ngome za makundi ya waasi mashariki mwa nchi hiyo katika eneo la milima ya mbuzi na Tchanzu iliyoko kaskazini mwa jimbo la Kivu.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa kutoka kwa jeshi hilo zinaeleza kuwa wapiganaji hao wanaomtii jenerali Jean Bosco Ntaghanda anayetafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC,wameweka ngome zao katika vijiji vya mpakani mwa Rwanda,Uganda na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Bosco Ntaghanda anatumia askari walioasi katika jeshi la nchi hiyo na kuendelea kufanya vitendo vinavyovunja haki za binadamu,ikiwemo mauaji na ubakaji.