SUDANI

Rais Omar Al Bashiri akiri haja ya kuwepo na amani baina ya Sudani na Sudani Kusini.

Rais wa Sudan Omar Al Bashiri amesema kuwa ipo haja ya kuwa na amani kati ya Sudani na Sudani Kusini na kwamba Sudani inadhamira ya dhati katika mikataba ya amani ambayo imesaini.

zesham.blogspot.com
Matangazo ya kibiashara

Akinukuu kauli ya rais Bashir, mpatanishi wa Umoja wa Afrika Thabo Mbeki muda mfupi baada ya kufanya mazungumzo na rais Bashir, amesema kuwa rais Bashir amekiri kuwepo haja ya amani baina ya mataifa hayo mawili.

Mkutano huo umekamilisha siku mbili za mazungumzo na maafisa wa Sudan huku Mbeki akijaribu kuzishinikiza Sudan na Sudan Kusini kurejea katika mazungumzo ambayo yalisitishwa baada ya kutokea mapigano katika mpaka mwezi uliopita.