SYRIA

Watu tisa wauwawa kwa shambulio la kujitoa mhanga nchini Syria.

Moja ya mashambulizi ya bomu yaliyotekelezwa nchini Syria
Moja ya mashambulizi ya bomu yaliyotekelezwa nchini Syria Reuters

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga ameua watu tisa jana Jumamosi Mashariki mwa Syria huku viongozi wa nchi nane zenye uchumi imara duniani G8 wakitoa wito wa mabadiliko ya kisiasa nchini humo na kutaka kumalizika kwa ghasia ambazo zimeua watu wanaokadiriwa kuwa elfu 12,000 hadi sasa.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao ambao ni pamoja na Urusi ambayo ni mshirika wa muda mrefu wa Syria imeitaka Syria kuongoza siasa za mpito ambazo zitasababisha kuwepo kwa demokrasia na mfumo wa vyama vingi.

Aidha viongozi hao wametoa wito kwa serikali ya Syria na pande zote kutii mara moja mpango wa umoja wa mataifa wa kukomesha mapigano na umwagaji damu nchini humo.