MAREKANI

Bunge la Marekani lapitisha vikwazo vipya dhidi ya Iran

REUTERS/Jason Reed

Bunge la Seneti nchini Marekani limepitisha vikwazo vipya dhidi ya Iran vinavyolenga kuishawishi Jamuhuri hiyo ya kiislam kuachana na mpango wake wa urutubishaji wa Madini ya Uranium.

Matangazo ya kibiashara

Mpango huo wa urutubishaji madini unapingwa na Marekani na jumuiya ya kimataifa hususan mataifa ya Magharibi yanasema kuwa umelenga kutengeneza silaha za Nyuklia.

Hatua hiyo ilipitishwa kwa pamoja wakati mataifa yenye nguvu duniani yakitarajia kukutana kesho mjini Baghdad nchini Iraq ambapo Iran itakuwa na wawakilishi katika mkutano huo.

Hatua hiyo pia imegusa yeyote yule aliyesaidia kwa hali na mali katika kufanikisha Iran kutengeneza Silaha za Nyuklia za Maangamizi.

Nayo Iran imeendelea kusisitiza kuwa mpango wake wa Nyuklia ni kwa ajili ya Matumizi yaliyo salama kwa ajili ya Raia wake.