Mali-Machafuko

Watu watatu wauawa nchini Mali wakati wa uvamizi wa waandamanaji kwenye Ikulu

Mei 21, wananchi wakiandamana kwenye mji mkuu Bamako baada ya kupatikana muafaka baina ya wanasiasa na ECOWAS
Mei 21, wananchi wakiandamana kwenye mji mkuu Bamako baada ya kupatikana muafaka baina ya wanasiasa na ECOWAS AFP/HABIBOU KOUYATE

Ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa UN umeonya kuwa Shambulio lilifanyika jana dhidi ya Rais wa Mpito wa Mali Dioncunda Traore lililotekelezwa na waandamanaji wenye hasira litakifanya kipindi hiki cha mpito kuwa katika hatari na kigumu.Watu watatu wameuawa nchini Mali wakati wa uvamizi kwenye ikulu ya rais nchini humo. Rais Dioncounda Traore alivamiwa na kundi la waandamanaji waliofaulu kumpiga hadi kumchania nguo.

Matangazo ya kibiashara

Juhudi za kidiplomasia zinazofanywa na jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Magharibi mwa Afrika, ECOWAS kushawishi viongozi walioongoza mapinduzi dhidi ya serikali ya nchi hiyo, kumkubali Traore ambaye ataongoza serikali ya mpito kwa kipindi cha mwaka mmoja, zimeingia katika hatari kutokana na matukio yanayotokea sasa.

Waziri wa mambo ya nje wa Cote d Ivoire ambaye hivi sasa ni mkuu wa ECOWAS amesema umoja huo hauungi mkono yaliyotokea nchini Mali na kutangaza kuwa muda mfupi ujao watatangaza hatua za kuchukua.

Rais wa mpito nchini humo, Dioncunda Traore alifikishwa hospitalini kwa ajili ya mapumziko baada ya waandamanaji wenye hasira wakipinga uteuzi wake walipovamia ofisi yake na kumpiga.

Nae Rais wa Ufaransa Francois Hollande akiwa katika mkutano wa nchi tajiri nchini Marekani amesema Ufaransa inafuatilia kwa karibu yanayojiri nchini Mali na kusistiza kuheshimiwa kwa mapendekezo ya ECOWAS.

saa chache tu baada ya wapatanishi kuondoka nchini Mali wakiwa na mawazo kuwa wameweza kuwashawishi viongoza waliiongoza mapinduzi dhidi ya Serikali ya Mali, kumkubali Traore, Maelfu ya Raia wa nchi hiyo waliandamana na kuvamia ofisi za Serikali mjini Kouluba.

Baada ya kipigo Traore alikimbizwa hospitali kufanywa uchunguzi na kubaini kuwa hali yake haikuwa mbaya na hivi sasa amepelekwa mahali penye usalama.