Mirsi-Uchaguzi

Wananchi wa Misri wapiga kura ya kumchagua rais wa baada ya utawala wa Hosni Mubarak

Ofisi ya kupigia kura
Ofisi ya kupigia kura REUTERS/Hani Abdulla

Wananchi milioni hamsini na mbili wa Misri wameanza kupiga kura mapema leo asubuhi katika uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika leo na kesho alhamisi kumchaguwa rais wao, ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu kuanguka kwa utawala wa rais Hosni Mubarak Februari 11, mwaka 2011.

Matangazo ya kibiashara

Ikiwa chini ya uongozi wa kijeshi tangu kuondolewa madarakani kwa utawala wa rais Hosni Mubarak, wananchi wa Misri wanamchaguwa rais wao leo na kesho na hivo kuamuwa hatma ya nchi hiyo inayo tawala na wanajeshi miaka hamsini na nane sasa.

Awali wagombea kumi na watatu ndio walikuwa kwenye orodha, hadi kipenga cha mwisho wamebaki kumi na wawili baada. Hata hivyo wagombea wanne ndio wanaokuja juu zaidi, ikiwa ni pamoja na Amr Moussa, Ahmed Chafik, Abdel Moneim Aboul Foutouh na Mohammed Morsi, wagombea wawili kati yao waliwahi kuhudumu katika utawala wa rais Hosni Mubaraka na wengine wawili ni kutoka upinzani wa chama cha Muslim Brodherhood.

Waangalizi zaidi ya elfu kumi wa kimataifa wapo nchini Misri akiwemo rais wa zamani wa Marekani Jimmy Carter kushuhudia uchaguzi huo wa kihistoria.

Katika kipindi cha miaka 58, Misri imekwisha tawaliwa na viongozi watatu na wote ni wanajeshi. Gamal Abdel Nasser (1954-1970), Anouar el-Sadate (1970-1981) na Hosni Moubarak (1981-2011)