IRAN-IRAQ

Iran yatishia kujitoa kwenye mazungumzo nyuklia, Yemeni yashambulia Al Qaeda

REUTERS/Thaier al-Sudani

Mazungumzo ya pande sita yenye lengo la kujadili utengenezaji wa silaha za nyuklia unaotekelezwa na serikali ya Iran umeingia siku ya pili nchini Iraq huku Tehran ikisema itajitoa iwapo itaendelea kutishwa. 

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Ujumbe wa Iran Saeed Jalili amesema nchi yake inataka Jumuiya ya Kimataifa iheshimu maslahi yao ikiwa ni pamoja na kulegeza vikwazo walivyoviweka dhidi yao na iwapo watashindwa kufanya hayo watajitoa kwenye mazungumzo hayo.

Tishio la kujitoa linakuja baada ya nchi hiyo kukubaliana na Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani IAEA .

Wakati huohuo Jeshi la Yemen limeendeleza mashambulizi yake dhidi ya Wanamgambo wa Al Qaeda wenye maskani yake nchini humo na kufanikiwa kuwaua wapiganaji thelathini na watano Kusini mwa Jimbo la Abyan.

Operesheni hii ya Kijeshi imeingia siku ya kumi na tatu ikiwa na lengo la kulitokomeza Kundi la Al Qaeda Tawi la Yemeni ambalom siku mbili zilizopita walitekeleza shambulizi la kujitoa mhanga na kuua wanajeshi tisini na sita waliokuwa kwenye mazoezi ya gwaride.

Afisa Mmoja wa Jeshi amesema walifanikiwa kuwaua wanamgambo hao thelathini na watano baada ya wao kuanzisha mashambulizi katika Mkoa wa Wadi Bani na ndipo wakaamua kujibu mashambulizi.