UFARANSA, AFGHANISTANI

Rais wa Ufaransa ataka majeshi yake yaondoke Afghanistan 2013

Rais wa Ufaransa Francois Hollande hii leo amefanya ziara ya ghafla nchini Afghanistan na kutemebelea kambi za jeshi la nchi yake walioko nchini humo kulinda amani.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Mara baada ya kuwasili rais Hollande alitembelea kambi ya jeshi ya mjini Kabul na kuwaambia wanajeshi wake kuwa msimamo wa kuviondoa vikosi vyote vya nchi hiyo uko palepale na mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2013 vitakuwa vimeondoka.

Rais Hollande pia amekutana na rais Hamidi Karzai na kufanya nae mazungumzo kuhusiana na mpango wa nchi yake kutaka kuondoa vikosi vyake nchini humo.

Hollande amewahakikishia wanajeshi wa nchi hiyo kuwa watakuwa wameondoka nchini humo mwaka 2013.

Hatua hiyo ya Hollande inapingana na mtazamo mwingine wa washiririka wa NATO ikiwemo Marekani ambao wanataka majeshi ya NATO yaondoke Afganistan ifikapo mwaka 2014.