DR CONGO

Jeshi la CONGO DR kupambana na waasi mashariki mwa Kivu

Wapiganaji waasi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo
Wapiganaji waasi wa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo nyenyerinews.org

Jeshi la serikali ya jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo limeendelea kupambana na waasi baada ya hali kuwa tete huko mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya mashambulizi ya mabomu hivi karibuni katika eneo la mipaka ya rwanda na uganda.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi hilo limekiri kukutana na upinzani mkali kutoka kwa waasi hao ambao wamekuwa wakijibu mashambulizi ya hatari.

Majeshi ya waasi nchini jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo yamejigamba jumamosi kuwa wamefanikiwa kujibu mashambulizi makali yaliyofanywa na majeshi ya serikali ya nchi hiyo huko mashariki mwa jimbo la Kivu.

Luteni kanali Vianney Kazarama, ambaye ni msemaji wa waasi alisema kuwa majeshi ya serikali yalitumia silaha kali wakijaribu kudhibiti eneo la Mbuzi na kushindwa baada ya kushambuliwa na kundi la waasi.