SYRIA

Umoja wa mataifa wathibitisha mauaji ya halaiki Houla,Syria.

waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague
waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague REUTERS/Francois Lenoir

Waangalizi wa Umoja wa mataifa wamethibitisha jumla ya maiti 90 zikiwemo za watoto 32 baada ya mashambulizi yaliyotekelezwa na majeshi ya serikali ya Syria.

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa mambo ya kigeni wa uingereza willium Hague amesema ni lazima kupatikane nguvu ya kimataifa kupambana na uhalifu uliokithiri kama wa Syria huku katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban ki Moon akisema ni wazi tukio hili linaonesha ukiukwaji wa sheria za kimataifa.

Wakati huohuo jeshi la Syria limeelekeza lawama kwa vikundi vya wapiganaji vya waasi.

Hili ni shambulio lingine lililogharimu maisha ya watu wengi wasio na hatia katika eneo la Houla tangu kuanza kwa rasha rasha za mapinduzi ya kutaka kumuondoa madarakani raisi wa Syria Bashar al Assad.