ISRAEL-PALESTINA

Israel yakabidhi miili 91 ya raia wa Palestina waliouawa kwenye mapigano

Serikali ya Israel imeanza kukabidhi miili tisini na moja ya raia wa Palestina waliouawa kwenye mashambulizi dhidi ya wale wanaoipinga Israel wakiwemo wengine waliouawa miaka arobaini iliyopita Mamlaka kutoka nchi zote mbili zimethibitisha.

Israel yakabidhi mabaki ya miili ya raia 91 wa Palestina ambapo imepelekwa Ramallah na Ukingo wa Gaza
Israel yakabidhi mabaki ya miili ya raia 91 wa Palestina ambapo imepelekwa Ramallah na Ukingo wa Gaza AFP PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa watu ambao waliuawa walikuwa wapiganaji wa Palestina ambao walikuwa wanapamba na utawala wa Israel katika miaka ya elfu moja mia tisa sitini na saba katika eneo la Ukingo wa Magharibi.

Miili hiyo ilianza kusafishwa mapema leo asubuhi ambapo imeshaanza kukabidhiwa kwa serikali ya Palestina ambapo miili sabini na tisa imeshapelekwa haraka kwenye Jiji la Ramallah na mingine kumi na mili imepelekwa Ukingo wa Gaza.

Makabidhiano ya miiili hiyo baina ya serikali ya Palestina na Israel yamefanyika katika Jiji la Jericho lililopo karib kabisa na eneo la Ukingo wa Magharibi kwa ajili ya shughuli za mazishi ambazo zimepangwa kufanyika haraka.

Mkuu wa Kamati ya Masuala ya Raia nchini Palestina Hussein Al Sheikh amesema wamekabidhiwa miili hiyo ambayo ilizikwa na serikali ya Israel kinyume cha ubinadamu na sasa wanafanyakazi ya kuzika upya.

Al Sheikh ameongeza kuwa miili hiyo yote imekabidhiwa ikiwa kwenye makasha maalum na kufunikwa bendera za Palestina ambapo zoezi la kutambua litafanyika kabla ya kuzika kwa taratibu za kidini.

Kamati ya Kijeshi ya Israel ambayo inafanyakazi na Kamati ya Masuala ya Raia ya Palestina imethibitisha shughuli hiyo inakwenda vyema licha ya kukiri bado hawajakamislisha zoezi la kukabidhi miili yote.