Nigeria

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan aahidi usalama wa safari za ndege

REUTERS/Akintunde Akinleye

Maafisa wa uokoaji nchini Nigeria wamekuwa wakiokota vipande vya miili ya watu 153 walioangamia katika ajali ya ndege iliyotokea Jumapili iliyopita mjini Lagos.

Matangazo ya kibiashara

Polisi wamelazimika kutumia gesi za kutoa machozi kuwasambaratisha idadi kubwa ya watu waliokuwa wamejitokeza katika eneo la ajali baada ya wao kuwa kikwazo kwa maafisa wa uokoaji kutekeleza majukumu yao.

Rais Goodluck Jonathan amesema serikali yake inaweka mikakati kabambe ya kuhakisha kuwa kuna usalama katika safari za ndege nchini humo ili kuzuia mkasa mwingine kama huo.

Uchunguzi unaendelea kubaini kiini cha ajali hiyo huku duru zikisema ajali hiyo ilisababitishwa baada ya ndege hiyo kukosa mafuta ya kutosha na kuharibu mitambo yake.

Serikali imetangaza siku tatu za kuomboleza kutokea kwa mkasa huo na bendera nchini Nigewia zinapepea nusu mlingoti.

Inahofiwa pia kuwa watu wengine wamepoteza maisha yao baada ya kuangukiwa na ndege hiyo,iliyoangukia majengo katika mji huo wenye idadi kubwa ya watu.

Mapema mwezi uliopita ndege nyingine ya kampuni ya Dana ilikumbwa na hitilafu ya kimitambo na kulazimika kutua mjini Lagos muda mfupi tu baada ya kupaa angani.
 

Idadi kubwa ya wasafari hutumia usafiri wa angaa kutoka uwanja wa kimataifa wa Murtala Mohammed mjini Lagos,kwenda katika mataifa mbalimbali katika mataifa ya Afrika Magharibi.