Syria-Urusi

Umoja wa Ulaya wataka Urusi kuunga mkono juhudi za kusitisha machafuko nchini Syria

Majeshi ya serikali nchini Syria yamekabiliana vikali na wapiganaji wa upinzani mjini Damascus.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini humo yanasema kuwa makabiliano hayo yalitokea jijini Damascus na Idlib na kusababisha kuuawa kwa wanajeshi 80 wa serikali.

Wakati hayo yakijiri,viongozi wa umoja wa Ulaya wanakutana mjini Saint Petersburg nchini urusi kuzungumzia hatima ya Syria, na wameafikiana kuweka nguvu zao pamoja ili kusaidia kumaliza machafuko hayo.

Rais wa Umoja huo Herman Van Rompuy amesema kuna umuhimu mkubwa wa Umoja huo kuungana na Urusi ili kuendelea kushinikiza mpango wa amani ulioandaliwa na msuluhishi wa mgogoro huo Koffi Annan.

Mkutano huu umekuja siku moja baada ya rais Bashar Al Assada kulihutubia bunge na kukanusha madai ya wapinzani na Umoja wa Mataifa kuwa serikali ilikuwa nyuma ya mauji ya zaidi ya watu mia moja katika mji wa Houla wiki moja iliyopita.

Rais Assad amedai mataifa ya Magharibi yanalengo kuibomoa nchi yake,na kungeza kuwa watu wa Syria watasimama na taifa lao ihadi mwisho.

Urusi na Uchina zimeenedelea kutumia kura zao za veto kupinga azimio lolote dhidi ya rais wa Syria Bashar Al Assad na washirika wake,kama inavyoshinikizwa na Marekani na mataifa mengine ya Umoja wa Ulaya.