Nigeria

Halmashauri ya safari za ndege nchini Nigeria yapiga marufuku kampuni ya ndege ya Dana

Tại hiện trường vụ tai nạn hàng không ở Nigeria, Iju-Ishaga, gần thành phố Lagos, 04/06/2012
Tại hiện trường vụ tai nạn hàng không ở Nigeria, Iju-Ishaga, gần thành phố Lagos, 04/06/2012

Halmashauri ya safari za ndege nchini Nigeria limesitisha leseni ya kampuni ya ndege ya Dana ilianguka siku ya Jumapili iliyopita na kusababisha vifo vya abiria 153 mjini Lagos.   

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa halmashauri hiyo Sam Adurogboye, amesema kwa sasa ndege za kampuni hiyo ya India hazitapaa katika angaa ya Nigeria hadi pale zitakazopewa leseni mpya,baada ya uthathmini mpya kufanyiwa ndege hizo.

Wakati hayo yakijiri, waokoaji wanaotafuta miili ya watu walioangamia baada ya kutokea kwa ajali ya ndege mjini Lagos nchini Nigeria mwishoni mwa wiki iliyopita, wanasema tayari wamepata miili 137 katika eneo la mkasa.

Waokoaji hao wanaongeza kuwa miili zaidi inatarajiwa kupatikana leo,pamoja na watu wengine ambao waliuawa baada ya ndege hiyo kuanguka Jumapili iliyopita.

Ndege hiyo aina ya kampuni ya Dana ilikuwa na abiria 153 kutoka Abuja kwenda Lagos wakati ilipoangukia makaazi ya majengo ya watu katika mji huo na kusababisha idadi ya watu wasiofahamika kuuawa.

Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan alizuru eneo la mkasa huo hapo jana, na kuahidi kuwa serikali yake itaweka mikakati ya kuimarisha safari za angaa baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Uchunguzi unaendelea kubaini kiini cha ajali hiyo,huku duru zikisema kuwa chanzo cha ajali hiyo kilitokana na mitambo ya ndege hiyo kuharibika.

Maafisa wa polisi tayari wamepata kifaa cha kunasa sauti ambacho kinasaidia kufanya uchunguzi zaidi kubaini hasa chanzo cha jali hiyo ambayo ni mbaya zaidi katika historia ya Nigeria.

Marekani kupitia kwa Waziri wake wa nchi za kigeni imetuma risasala za rambirambi kwa serikali ya Nigeria kutokana na ajali hiyo.

Marekani imesema kuwa iko tayari kusaidia katika uchunguzi wa kubaini lengo la ajali hiyo.