Uingereza

Malkia Elizabeth wa II aadhimisha miaka 60 kama Malkia wa Uingereza

REUTERS/Andrew Winning

Hatimaye hafla ya kuadhimisha miaka 60 ya Malkia wa Uingereza Elizabeth wa II , imekamilika leo jijini London na kuhudhuriwa na maelfu ya raia na wageni wengine mashuhuri kutoka ndani na nej ya nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Malkia Elizabeth ameadhimisha shehere hizo bila ya mumewe Prince Philip mwenye umri wa miaka 90 ambaye amelazwa hospitalini baada ya kuugua gafla.

Shehere hizo pia zilihudhuriwa na wanasiasa mbalimbali nchini humo pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali ambao pia walihudhuria ibada katika kanisa la Kianglikana la Mtakatifu Paulo jijini London kumshukuru Mungu kwa kipindi hicho chote ambacho Malkia Elizabeth wa II amekuwa kiongozi wa taifa hilo.

Akizungumza na wananchi wa Uingereza akiwa kanisani Malkia Elizabeth alisema alikuwa na furaha kubwa kuadhimisha miaka 60 kama kiongozi wa nchi hiyo na kumwomba kila mmoja kumwombea mumewe Prince William ili apate nafuu.

Baadhi ya walioshuhudia hafla hiyo walisema walisikitishwa na kutokuwepo kwa Prince Charles ambaye siku zote amekuwa pembeni pa Malkia katika ziara na sherehe mbalimbali.